Xara graphics software

12:17
1

Oprah Winfrey

Orpah Gail Winfrey ndilo jina alilopewa na wazazi wake mama huyu lakini kutokana na watu kushindwa kutamka vizuri neno ORPAH kwa kutamka OPRAH badala yake, mama huyu aliamua kutumia jina hili moja kwa moja.

Oprah Winfrey ni mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya Afrika ( African American ), alizaliwa mnamo January 29, 1954 huko Mississippi, Marekani katika familia ya kimaskini na iliyojawa na adha kubwa ya maisha kwa wakati huo. Mafanikio ya Oprah, ndiyo yaliyonifanya kumdadisi zaidi na kufahamu storia yake kwa ufupi kwa ajili ya kujifunza na kupata changamoto kutoka kwake.

OPRAH WINFREY
Oprah, ama maarufu kwa jina la Lady O, ni mwanamke mrembo akiwa na urefu wa 1.69m uliomuwezesha kushinda taji la Miss Black Tennessee beauty pageant akiwa na umri wa miaka 17 tu. Kitu ambacho pengine ulikuwa hujui, Lady O ni muhanga wa mimba za utotoni, kwani alipata mimba akiwa na umri wa miaka 14 tu na kwa bahati mbaya mtoto wake alifariki alipojifungua.

Licha ya changamoto zote hizo alizozipitia  Lady O, lakini kwa sasa ana nyadhifa zifuatazo:

  • Mwenyekiti, CEO na CCO wa The Oprah Winfrey Network ( OWN )
  • Mwenyekiti na CEO wa Harpo Productions.
  • Mwanzilishi wa O, The Oprah Magazine


Oprah ni maarafu kwa kipindi chake cha The Oprah Winfrey talk show ambacho ndo kimempa umashuhuri mkubwa sana duniani, Oprah ni mtayarishaji, mtangazaji na muigizaji maarafu ambaye ni kioo kwa kila mwanamke na hata mwanaume anayepigana kupata mafanikio.

Kubwa zaidi kuliko yote ambalo limenivutia zaidi ni kwamba huyu ndiye mmarekani mweusi tajiri kuliko wote ( richest african american ) ndiyoo..ni mwanamke...amewapiku kina Michael Jordan, kina Lebron James na wengine weeeeengi, yeye ndo kinara akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia US dollars 2.9billion ambazo ni sawa na trillion 6.5 za kitanzania..yaaah..kwa hapa bongo angekuwa nambari moja kwani hata MO anautajiri wa US Dollars 1billion tu.

Oprah amejitoa kwa jamii hasa kwa watoto wa kike kwa kufungua shule ya uongozi iitwayo The Oprah Winfrey Leadership Academy for girls ambayo ipo Afrika ya kusini na ilifunguliwa mnamo mwaka 2007.
Lady O ni mama lakini licha ya umri wake wa miaka 63 hadi sasa hana mtoto na hataki kuwa mama.

Huo ndo wasifu mfupi wa Oprah ambao kwa namna moja ama nyingine inaweza kuwa kama changamoto kwa vijana kufikia safari ya mafanikio yetu.


1 comments:

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....