Ma Yun
Ndilo jina halisi Ma Yun maarufu kama Jack Ma, mzaliwa wa China kaunti ya Hangzhou, Zheijang. Alizaliwa Septemba 10, 1964 ( miaka 53 iliyopita ).
Ma Yun |
Ma Yun ndio mtu tajiri zaidi katika bara la Asia akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola za kimarekani 41.8 billion na anashika nafasi ya 14 katika orodha ya matajiri 2043 duniani liyotolewa na forbes mwaka 2017. Utajiri wake unatokana kwa kiasi kikubwa na kampuni yake ya Alibaba ilioanzishwa mwaka 1999 bonyeza hapa kuona zaidi kuhusu alibaba
Ma Yun alikulia katika mazingira magumu ya kielimu,kwani alikuwa hana uwezo mkubwa wa kitaalumu hivyo perfomance yake darasani haikuwa nzuri na alikariri mtihani mara kwa mara ili kuweza kufaulu. Hiyo haikumkatisha tamaa, kwani alitumia muda mwingi sana kujifunza lugha ya kiingereza kwa takribani miaka 9, alikuwa akijichanganya na wageni na kuzungumza nao ili kujifunza zaidi kiingereza na ndipo alikutana na mtalii mmja ambae alimpa jina la Jack kwa sababu alishindwa kutamka Ma Yun kiurahisi.
Mwaka 1988 alipata Bachelor of Arts in English katika chuo cha Hangzhou Teacher's Institute na baada ya hapo alijaribu kutafuta kazi lakini hakufanikiwa.
Ma anasema, "I even went to KFC when it came to my city, 24 people went for the job. Twenty three were accepted. I was the only guy....".
Alijaribu kuomba kazi Harvard mara 10 lakini alikataliwa mara zote.
Mwaka 1994 Ma alipata habari kuhusu internet, mwaka 1995 alienda USA na marafiki zake walimsaidia kuhusu mtandao na mwaka huohuo yeye na rafiki zake walifungua ukurasa uliokuwa unaitwa China Yellow Pages na ndani ya miaka mitatu walikusanya takribani USD 800,000.
Akiwa na miaka 33, kwa mara ya kwanza Ma ndo alimilika kompyuta yake, akiwa na ujuzi mdogo kabisa wa coding, leo hii ana miliki mtandao mkubwa wa online sales. Hii ni changamoto kwa vijana wetu, Ma alitumia nafasi hiyo hiyo ndogo aliyokuwa nayo kwenye mtandao kufanya vitu vikubwa. Ma anasema:
"the day we got connected to the web, I invited friends and TV people to my house, and on a very slow dial-up connection we waited three and a half hours and got half page....we drank, watched tv and played cards, waiting. But I was so proud. I proved the internet existed."
Kwa sasa Ma ni mtu mashuhuri sana, ni mjasiriamali mkubwa sana akiwavutia vijana wengi sana katika hustle za maisha. Amekuwa akialikwa kufundisha vyuo mbalimbali vikiwemo Harvard na Pennsylvania, inashangaza kwa kweli, wakati huo aliomba kazi Harvard akakosa, sahivi wanamtafuta wao. Big Inspiration.
Hiyo ndo historia fupi tu ya Jack Ma, mwanzilishi wa ALIBABA GROUP..
Shukrani.
0 comments:
Post a Comment
Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.