Xara graphics software

10:56
3

Karibu mpendwa msomaji, ni wakati mwingine tena ambapo tunaendelea na orodha ya matajiri duniani mwaka 2017 kama ilivyotolewa na Forbes March 20, 2017

Kati ya matajiri wote walioorodheshwa 2043, ni wanawake 227 pekee ambao ni sawa na 11% ya matajiri wote. Hili ni ongezeko kubwa kutoka wanawake 202 mwaka 2016 mpaka kufikia wanawake 227 mwaka huu. Jumla ya mapato ya wanawake hawa 227 ni sawa na US Dollars 852.8billion ambazo ni sawa na trillion 1901.664 shilling za kitanzania. Wengi wa matajiri hawa wakike wamepata utajiri wao kwa kurithi kutoka waume zao au wazazi wao, japokuwa wapo pia waliojitengeneza wenyewe.

Real Women

Ifuatayo ni orodha ya wanawake watano matajiri zaidi duniani.

1. LILIANE BETTENCOURT

Huyu ndiyo mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia US Dollars 39.5billion ambazo ni sawa na trillion 88.16 shilling za kitanzania, hii ni sawa na mara 3 ya bajeti ya Tanzania mwaka 2017/2018.

Liliane Bettencourt

 Liliane alizaliwa Octoba 21, 1922 akiwa na umri wa miaka 94 mpaka sasa. Ni raia wa Ufaransa na chanzo cha utajiri wake ni kampuni ilioanzishwa na baba yake mwaka 1907 ya L'Oreal.


2. ALICE WALTON

 Alice ana utajiri unaofikia US Dollars 33.8billion ambazo ni sawa na 75.44trillion shilling za kitanzania, hii ni sawa na mara 2 ya bajeti ya Tanzania 2017/2018.

ALICE WALTON

Alice ni mmja wa binti za mzee Walton Mart, familia ya mzee Walton imetoa mabinti wa 4 kwenye orodha ya wanawake 227. Alice alizaliwa October 7, 1949 ana umri wa miaka 67 mpaka sasa. Elimu yake ya juu ameipata kutoka chuo kikuu cha Trinity, na utajiri wake unatokana na kampuni yake ya Llam pamoja na Walmart.

3. JACQUELINE MARS

Akiwa na umri wa miaka 77 tu mpaka sasa, Mars ana utajiri unaofikia US Dollars 27billion ambazo ni sawa na 60.3trillion shilling za kitanzania.


JACQUELINE MARS
 Jacq ni  mzaliwa wa Marekani, alizaliwa October 10, 1939. Chanzo kikuu cha utajiri wake ni kampuni ya Mars Inc ilioanzishwa mwaka 1911.

4. MARIA FRANCA FISSOLO

Mama huyu ana utajiri unaofikia US Dollars 25.2billion ambazo ni sawa na trillion 56 shilling za kitanzania kwa sasa.

MARIA FRANCA FISSOLO

Kwa sasa Maria ana umri wa miaka 76, ni raia wa Italia na utajiri wake unatokana na kampuni ya Ferrero Group iliyoachwa na marehemu mumewe Michel Ferrero.

5. LAUREN POWELL JOBS

 Akiwa na umri wa miaka 53 tu, mama huyu  wa kimarekani ana utajiri unaofikia US Dollars 20billion ambazo ni sawa na 44.64trillion shilling za kitanzania.

LAUREN POWELL JOBS

Mama huyu aliezaliwa Novemba 6, 1963 ni mjane wa Steven Jobs ( mwanzilishi wa Apple ) na utajiri wa huyu mama unatokana na hisa zake kwenye kampuni ya Apple.


Kitu cha kuvutia kwenye orodha hii ni kwamba top 3 wote wamezaliwa October, sio hao tu kuna watu wengi mashuhuri wenye mafanikio duniani waliozaliwa Octoba, sijajua kuna nini mwezi Octoba, lakini naweza kusema kwamba ni mwezi wa watu wenye mafanikio sana.
Asante kwa kuungana nami mpendwa msomaji, usisite kuacha maoni yake kuhusiana na chochote kile.
Asante.

3 comments:

  1. Asee very interesting to hear about them..dey make me struggle

    ReplyDelete
  2. Je unasumbuliwa na umaskini, mapenzi au ndoa, wizi wa mali, dhuruma na mengineyo.....

    UTAJIRI AU MALI NDANI YA MASAA 48 KWA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MCHACHE KIKUBWA UWE NA NIA YA DHATI.

    CALL/WHATSUP +255 742162843
    HATA UKIWA NJE YA NCHI POPOTE INSHAALAH HUDUMA INAKUFIKIA


    Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dua Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi?


    NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI MPAKA MASAA 72(SIKU 3) PAPO HAPO ULIPO KUPITIA KALAMA KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......



    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA



    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843


    HACHA KUTANGATANGA PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI



    NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI NA KUTUNZA SIRI......



    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)

    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.


    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA YA DHATI

    ReplyDelete

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....