Xara graphics software

12:31
0

Universities Ranking

Karibu tena kwenye jukwaa hili na leo nimeona tuangalie orodha ya vyuo vikuu bora kwa mwaka wa masomo 2017/2018.


Image result for graduates
               QS World University rankings pamoja na Times Higher Education World University rankings imekuwa mitandao inayoaminika kwa kutoa tathimini ya vyuo vikuu duniani kote. Orodha ya leo imehusisha data zilizotolewa na QS World University rankings kwa mwaka huu 2017. Vyuo vikuu takribani 1000 vimeshirikishwa na mtandao huu. Vyuo hupimwa kwa mambo kama:


  • Majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa
  • Maoni ya wasomi pamoja na waajiri
  • Ushiriki wa vyuo vikuu katika ngazi ya kimataifa
Image result for harvard university
Harvard University

            

              Baada ya kuangalia mambo hayo, orodha ya vyuo vikuu bora duniani kwa mwaka 2017/2018 ni kama ifuatavyo (10 bora tu) :



  1. Massachusetts Institute of Technology (kutoka Marekani)
  2. Stanford University (kutoka Marekani)
  3. Harvard University (kutoka Marekani)
  4. California Institute of Technology (kutoka Marekani)
  5. Cambridge Univesity (kutoka Uingereza)
  6. Oxford University (kutoka Uingereza)
  7. University College of London (kutoka Uingereza)
  8. Imperial College of London (kutoka Uingereza)
  9. Chicago University (kutoka Marekani)
  10. ETH Zurich (kutoka Uswisi)
              Katika orodha ya 200 bora, ni chuo kimoja tu pekee kutoka Afrika ambacho ni University of Cape town. Katika orodha nzima ya vyuo 1000 bora duniani, kutoka Afrika ya Mashariki ni vyuo viwili tu vimeweza kuingia ambavyo ni Makerere University kutoka Uganda na University of Nairobi kutoka Jamhuri ya Kenya.


Related image
Wahitimu wa Makerere University

               Kwa upande wa bara la Afrika, ifuatayo ni orodha ya vyuo vikuu bora kabisa kwa mwaka 2017/2018:



  1. University of Cape Town  (nafasi ya 191 kwa ubora duniani)
  2. Stellenbosch University kutoka Afrika ya Kusini (nafasi ya 361 duniani)
  3. University of Witwatersrand kutoka Afrika ya Kusini (nafasi ya 364 duniani)
  4. The American University in Cairo kutoka Misri (nafasi ya 395 duniani)
  5. Cairo University (nafasi ya 481 mpaka 490 duniani)
  6. University of Pretoria kutoka Afrika ya Kusini
  7. University of Johannesburg kutoka Afrika ya Kusini
  8. Ain Shams University
  9. Rhodes University kutoka Afrika ya Kusini
  10. University of Kwazulu-Natal
  11. Alexandria University (Misri)
  12. Al-Azhar University
  13. Makerere University (Uganda)
  14. Northwest University
  15. University of Mohammed V de Rabat (Morocco)
  16. University of Ghana
  17. University of Nairobi
  18. University of Western Cape.
              Kwa mshangao mkubwa kabisa vyuo kutoka Tanzania havipo kwenye orodha ya vyuo vikuu bora kwa mwaka 2017, na madhara ya hili ni nafasi finyu kwenye ushindani wa ajira ukilinganisha na wenzetu wa Kenya na Uganda.

Hope Umeenjoy kusoma thread hii, shukrani kwako. Usisahau kukoment, na kupenda page yetu ya facebook @thefontyn.



0 comments:

Post a Comment

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....