Xara graphics software

07:39
0

Robert Gabriel Mugabe

         Robert Gabriel Mugabe kwa sasa ndiye rais mwenye umri mkubwa kuliko marais wote duniani, akiwa na miongo 9, mzee huyu kwa kweli amekula chumvi nyingi sana. Kilichonivutia sio umri wake mkubwa bali ni elimu yake. Mhe.Mugabe ndiyo rais mwenye elimu kubwa kuliko wote mpaka sasa akiwa na shahada 18 tofauti tofauti na alizozipata kutoka katika vyuo mbalimbali duniani.

Image result for robert mugabe
Robert Gabriel Mugabe
                Rais Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 (miaka 93) huko Kutama, Southern Rhodesia kwa wakati huo, lakini sahivi tunaitambua kama Zimbabwe. Maisha yake hayakuwa mazuri kwa wakati huo kwasababu bado walikuwa wakitawaliwa na wakoloni na Mzee Mugabe kama jinsi ilivyo kwa viongozi wengi wa ukombozi wa Afrika, alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanajipatia uhuru. Harakati hizi kwa wakati fulani zilimsababishia kuwekwa jela kwa miaka 11. Haikuwa shida kwake kwasababu wakati yupo jela bado aliendelea na harakati nyingine. Kitu kizuri kumuhusu Mugabe ni kwamba anapenda sana elimu, wakati alipokuwa jela alitumia muda mwingi kusoma na hatimae alipata shahada mbili wakati yupo huko.
Image result for robert mugabe

            Mpaka sasa Mugabe ana degree 18 ambazo kati ya hizo:shahada 6 ni za distance learning na mbili akiwa gerezani. Baadhi ya vyuo ambavyo Mugabe amepatia hizo shahada ni:
  1. University of London
  2. Fort Hare University kutoka Afrika ya Kusini
Na vyuo vingine vingi kutoka pande tofautitofauti za dunia ambavyo vimempatia shahada za heshima. Baadhi ya shahada ambazo Mugabe anazo ni:
  • Bachelor of Arts (History and English)
  • Bachelor of Administration
  • Bachelor of Education (kwa wakati fulani Mugabe alikuwa mwalimu)
  • Bachelor of Laws from University of London
  • Masters of Laws from University of London
  • Master of science in Economics from University of London
Na nyingine nyiiiingi tu. Mugabe ameshika nyadhifa tofautitofauti mbali na uraisi tangu 1987 ambazo ni:
  • Waziri mkuu wa Zimbabwe (1980 - 1987)
  • Katibu mkuu wa Non-Aligned Movement (NAM)
  • Mwenyekiti wa 13 wa Umoja wa Afrika
Image result for robert mugabe

Huyo ndo Mzee Mugabe, akiwa na umri wa miaka 93 bado ana nguvu za kugombea uchaguzi unaofuata wa Zimbabwe. Ni kiongozi wa mfano kwa jamii ya Afrika.

Thank You.

0 comments:

Post a Comment

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....