Xara graphics software

05:33
0

              Kusurf mtandaoni, kuangalia vipindi unavyovipenda kutoka katika channels tofauti tofauti za tv ni jambo la kawaida kwetu, lakini kwa Korea sivyo kabisa.

             Democratic People's Republic of Korea (DPRK) Korea ya Kaskazini, taifa la kikomunisti na la kidemokrasia kama jinsi katiba ya nchi hiyo inavyosema ni taifa linalopatikana katika peninsula ya Korea, mashariki mwa Asia. Peninsula ya Korea imegawanyika sehemu mbili ambazo ni Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini, lakini Korea ya Kaskazini inatumia jina la Korea na sio Korea ya Kaskazini kama wengi wetu tunavyojua kwa kuwa wanaamini sehemu ya kusini ya Korea ambayo inaongozwa na Rais Moon-Ja ni koloni la Marekani.

           Kuna mambo mengi sana ya kustaajabisha ukiwa Korea ya Kaskazini (DPRK), mambo ambayo pengine kwetu sisi ni mambo ya kawaida lakini huko ni tofauti kabisa. Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo:
  1. Ni taifa lenye usiri mkubwa sana
Usiri wa hali ya juu unapatikana DPRK, kwa taarifa yako kiongozi wa sasa wa DPRK, Kim-Jong Un (supreme leader) tarehe yake ya kuzaliwa na mwaka halisi haijulikani. Inasemekana alizaliwa kati ya 1983 au 1984. Kuzungumzia jambo hilo ukiwa Korea ya Kaskazini huruhusiwi kabisa.

Image result for KIM JONG UN
    


    2. Hakuna huduma ya internet
Nafikiri hili ni jambo baya sana kwa wakazi wa DPRK, hawana huduma ya internet na hairuhusiwi kuingia mtandaoni kwani serikali inafikiri watu watajifunza tamaduni za kimagharibi na kuvunja sheria za nchi hiyo. Internet inapatikana kwa viongozi wa juu tu ambao wameruhusiwa kufanya hivyo.
Related image

  

 3. Huu ni mwaka 105 na sio 2017.
Usishangae, ndivyo ilivyo. Kwa Korea ya Kaskazini huu ni mwaka 105 na sio 2017. Mwaka ulianza kuhesabiwa baada ya kuzaliwa kwa Rais wa Milele wa Korea ya Kaskazini, Kim Il Sung. Kim Il Sung alizaliwa mwaka 1912 na kufariki mnamo mwaka 1994. Yeye ndiyo Mwanzilishi wa DPRK na ndiyo Rais wa kwanza na wa milele (eternal leader) wa DPRK. Kwa sasa hamna cheo cha Rais huku Korea ya Kaskazini kwa sababu Rais ni Kim il Sung japokuwa ameshafariki miaka 23 iliyopita.

Image result for 105 year in north korea
   

    4. Adhabu kwa Vizazi vitatu ( three generations punishment )
Jambo la kusikitisha zaidi, kosa akifanya mtoto hadi mzazi atahusika na adhabu. Vizazi vitatu maana yake Baba, Mtoto na Mjukuu wote watahusika na adhabu kwa kosa la mmoja wapo. Daaah hii ingekuja bongo sijui kama nafasi zingetosha kweli huko magerezani..!!!!

Image result for three generation punishment in north korea
    


     5. Kuna channels 3 tu za runinga
Nchi ya kidemokrasia au kidomokrasia???? Sijui, ila huu ni udikteta uliopitiliza. Wananchi wanaruhusiwa kuangalia channel 3 tu za runinga ambazo zote zinaendeshwa na serikali. Mbili hurusha matangazo yake kila siku lakini jioni tu. Na nyingine hurusha matangazo yake siku za week-end tu.
Image result for three tv channels in north korea

   6. Kuna aina 28 tu za kunyoa nywele
Mwaka 2013, kiongozi wa DPRK, Kim Jong Un alipitisha aina 28 tu za kunyoa nywele, aina nyingine haziruhusiwi kabisa. Cha ajabu aina ya unyoaji ya Kim Jong Un haikujumuishwa kwenye hizo 28 ikiwa na maana ya huruhusiwi kunyoa kama Kiongozi Kim Jong Un.


  7. Jeans ni marufuku
Haha..!!! kwa wale wapenzi wa jeans, huwezi kuishi DPRK kwani hairuhusiwi kuvaa jeans, ni kosa kisheria kuvaa jeans kwani inasemekana jeans zimetoka Marekani na Marekani ni adui mkubwa wa Korea ya Kaskazini.

Image result for no jeans in north korea
  

       
     8. Lazima upate kibali kutoka serikalini ili uweze kuishi Pyongyang
Pyongyang ni mji mkuu wa DPRK, mjii huu ni kwa ajili ya watu maalum, sio kila mtu anaweza kuishi. Pyongyang ni kwa ajili ya matajiri na wasomi, watu wenye nyadhifa kubwa serikalini, hivyo huruhusiwi kuishi Pyongyang bila ruhusa.
Image result for pyongyang in north korea

  


        9. Hairuhusiwi kuendesha gari kwa mtu wa kawaida
DPRK ni sehemu ambayo haina traffic lights na hii ni kwa sababu idadi ya magari ni ndogo kupita kiasi, kwani inasemekani kati ya watu 1000 ni mtu mmja tu au asiwepo hata mmoja anayemiliki gari. Magari humilikiwa na serikali na matajiri wakubwa ambao wana nyadhifa kubwa serikalini.
Image result for traffic lights in north korea

  


       10. Kumiliki Biblia ni kosa kisheria
DPRK haina dini, na wananchi wake pia hawana dini. Kuonekana ukifanya shughuli yeyote ya kidini hasa dini za kimagharibi kama vile Ukristo na Uislamu ni kosa kisheria.

  11. DPRK ina uwanja mkubwa kuliko wowote ule duniani
Jambo zuri kuhusu DPRK ina uwanja ambao una uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 150, 000 kwa wakati mmoja. Na hii imevunja rekodi kwani hakuna sehemu nyingine duniani yenye uwanja mkubwa kama huo.

  12.Miili ya Kim Jong Il na Kim Il Sung mpaka leo ipo
Miili yao imehifadhiwa na watalii wanaruhusiwa kwenda kuiangalia na kutoa heshima.


Yapo mengi sana ambayo ni ya kitofauti sana na dunia yetu ya kawaida, Muasisi wa DPRK Kim Il Sung anaonekana kama ndo mungu wao, picha za Kim Il Sung pamoja na Kim Jong Il zipo kila nyumba, kila mahali na  lazima utoe heshima mbele ya picha hizo. Achana na hiyo, jamaa wanapenda basketball ila wana sheria zao za kipekee kabisa, ila ambacho ulikuwa hukijui sasa DPRK ilijiunga na umoja wa mataifa UN mwaka 1991.


ASANTE....!!!!!

0 comments:

Post a Comment

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....