Dr.Jakaya Mrisho Kikwete
JK akiwa kwenye sare za jeshi. |
JK ni moja ya viongozi wanaopendwa sana barani Afrika, kwani kwa ripoti za 2013 alikuwa kiongozi wa sita anaefuatiliwa na watu wengi sana kwenye twitter. JK ni kiongozi mcheshi na aliyekuwa karibu na wananchi wake tofauti na viongozi wengine wa Afrika. Hakika ni mfano mzuri wa kuigwa kwa vijana wetu na watoto wetu wenye ndoto za kufikia malengo yao ya ama kuwa kiongozi wa nchi au mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa jamii.
JK |
Historia ya JK inaanza kijiji cha Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, mnamo Octoba 7, 1950 Rais wa awamu ya nne wa TZ alizaliwa. Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya Karatu Primary School na Tengeru School ( 1959 - 1965 ). Elimu ya Sekondari aliipata Kibaha Secondary School (o level 1966 - 1969) na Tanga Technical School ( advanced level ). Baadae alijiunga na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam na alihitimu elimu yake akiwa na degree ya Agrieconomics mwaka 1975.
JK alipata nafasi ya kuhudumu katika serikali kwenye nyadhifa tofautitofaut, mwaka 1994 alikuwa waziri wa Fedha akiwa na umri wa miaka 44 tu, alikuwa waziri mdogo kuliko wote kwa wakati huo. Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje na aliekuwa Rais wa awamu ya tatu Mhe. Willium Mkapa. Alihudumu katika nafasi hiyo mpaka mwaka 2005 alipopata nafasi ya kuingia ikulu kama Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
![]() |
JK akiwa na Harmonize. |
Kama nilivyosema hapo awali JK ni moja ya mifano ya kuigwa kwa vijana wenye ndoto za kuja kuwa kama yeye, kwanza ni msomi, mtu mkarimu, mwenye nidhamu ya kazi tusisahau kwamba JK pia alikuwa mwanajeshi na alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Kanali. TZ imeshuhudia mabadiliko makubwa sana wakati wa utawala wake kwenye sekta mbalimbali nyeti ikiwemo elimu. Tunakukumbuka sana JK kwa kutuletea shule za kata ambazo zimetusaidia sana ikiwemo mimi pia ambaye ni zao la shule ya kata ( Mtakuja Beach Secondary School ).
Kimataifa, JK amewahi shika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ( 2008 - 2009 ), pia mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama SADC ( 2012 - 2013 ).
Mbali na hayo, JK amepokea tuzo mbalimbali za heshima kwa ajili ya mchango wake ndani na nje ya Tanzania.
Huyo ndo JK kwa ufupi tu. Tunaheshimu mchango wako na ni wa kukumbukwa vizazi na vizazi.
Asanteni.
������ interesting
ReplyDeleteThat's fantastic Ray.....keep it up itbis interesting
ReplyDeleteGreat
ReplyDeleteThank you Jackson Ngasi
Delete