Mafanikio yeyote yale huwa ni matokeo ya kuzikabili changamoto ambazo humpata mtu kwa wakati ambapo anayatafuta mafanikio hayo. Changamoto ni vikwazo vinavyojitokeza kwenye njia yote ya mafanikio na hazina budi kujitokeza ili iweze kuwa fundisho na mfano hai kwa watu wengine.
Changamoto huweza kumjenga mtu au kumkatisha mtu tamaa kwa kiasi kikubwa sana kama atakosa mtu wa kumshauri.
Tunaweza kujifunza umuhimu wa kuzikabili changamoto kutoka kwa baadhi ya watu walioweza kuzikabili na kufanikiwa kwa kiasi chao. Mfano mzuri ni Abraham Lincoln pamoja na Michael Jordan. Watu hawa walipitia vikwazo vingi sana katika safari ya mafanikio yao. Unaweza kuangalia biography yao kwenye wikipedia hapo pembeni.
Unajifunza nini kutokana na changamoto ulizonazo?? Je changamoto zimekuwa mlima mkubwa sana kwako??? au umezitumia kama daraja ili kuweza kufikia mafanikio yako???
Weka mchango wako hapa chini tuweze kwenda sawa na maada hii..
SO GOOD
ReplyDelete