Xara graphics software

12:21
0

  Karibu tena ndugu msomaji, ni siku nyingine tena njema tuliyopewa na Mungu Mwenyezi, leo tunakwenda kuangalia list ya matajiri kumi (10) wakubwa duniani kulingana na taarifa iliyotolewa na gazeti la Forbes, March 2017.

Mabilionea wa dunia.

 Kama ilivyokawaida ya Gazeti la biashara la nchini marekani kutoa list ya majina ya watu matajiri dunian, list hiyo pia imetoka mapema mwezi huu March 2017 ikionyesha ongezeko kubwa la matajiri duniani kutoka matajiri 1810 mwaka 2016 mpaka kufikia matajiri 2043 mwaka huu 2017.

 Repoti hiyo inaonyesha uwepo wa majina mapya 195 miongoni mwao 76 wakiwa kutoka China na 25 kutoka USA. Katika idadi hiyo ya matajiri 2043 ambayo ni idadi kubwa ya watu matajiri kuwahi kuandikwa tangu Forbes ilipoanza kazi hiyo mwaka 1987, wanawake ni 227 tu.

  Kiwango cha jumla ya mapato ya matajiri hawa kimeongezeka kutoka dola za kimarekani trillion 6.5 ( ambayo ni sawa na trillion 14508 TZS ) mpaka kufikia dola za kimarekani trillion 7.67 ( ambayo ni sawa na trillion 17119.944 TZS ). Mapato ya mabilionea hawa yameongezeka kwa kasi sana kutoka US dollar trillion 1 mwaka 2000 mpaka kufikio US dollar trillion 7.67. Huku watanzania tukizidi kulia njaa na kumlalamikia Rais kwamba amebana pesa, wenzetu wanazidi kujiimarisha kiuchumi wakiongeza mikwanja mirefu tu kila siku.

  Kwa uchache, orodha ya matajiri ( mabilionea ) kumi 10 wa mwanzo ni hii hapa...

1. BILL GATES

  Bill Gates ana utajiri unaofikia US dollars 86billion ambazo ni sawa na trillion 191.952 za kitanzania.
Bajeti ya Tanzania mwaka 2017/2018 ni trillion 31 TZS, kwa maana hii sasa Bill Gates ana utajiri ambao ni sawa na mara 6 ya bajeti ya Tanzania.

                             Bill Gates
 Bill Gates ni raia wa Marekani, ana umri wa miaka 60 sasa, na utajiri wake unatoka na Microsoft.


2. WARREN BUFFET

 Warren Buffet ana utajiri unaofikia US dollars 75.6billion ambazo ni sawa na trillion 168.7392 za kitanzania.
Kwa utajiri huu anauwezo wa kulipia bajeti yote ya serikali kwa muda wa miaka 5 mfululizo. Huku sisi na serikali yetu tukihangaika kutafuta misaada kwa ajili ya hizo trillion 31, kuna mtu ana ona hizo ni hela za mboga tu..


WARREN BUFFET

Buffet ana umri wa miaka 85 na ni raia wa Marekani. Chanzo kikuu cha utajiri wake ni kampuni yake ya Berkshire Hathaway.


3. JEFF BEZOS.

Bezos ana utajiri unaofikia US dollars 72.8billion ambazo ni sawa na trillion 162.45 shilingi za kitanzania, ina maana kwamba ni  mara 5 ya bajeti ya Tanzania.

JEFF BEZOS

Bezos ana umri wa miaka 53 tu na ni raia wa marekani, utajiri wake unatokana na Amazon.com

Hiyo ndio tatu bora kwa sasa ya matajiri duniani, tutaendelea mpaka kumi bora yote. Pia tutaangalia kati ya matajiri hao 2043 ni akina nani wanatoka Afrika na je Tanzania imetoa matajiri wangapi kwenye orodha hiyo.
Usisite kuungana nami kwa kutembelea blog hii kila siku kwa mambo mazuri ya kusisimua na ya kukupa shauku ya mafanikio...

0 comments:

Post a Comment

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....