Hakika kama kungekuwa na njia rahisi ya mafanikio, basi kila mtu angekuwa ameshafanikiwa..lakini sivyo, Mafanikio yana njia ngumu sana iliyo jawa na misukosuko na changamoto nyingi ambazo tukiweza kushinda tunafanikiwa kwa hakika.
Mafanikio ni kupata unachokitaka na kukosa ambacho hukitaki. Sisi binadamu tunawaza mambo mengi sana ambayo ni mema na mengine ni mabaya, kati ya hayo tunayoyawaza na kuyafikiria, kwa vyovyote vile tukiweza kutimiza basi hiyo ndio maana ya mafanikio. Ukipanga kuiba na usikamatwe na ukaweza kuiba bila kukamatwa hayo ni mafanikio, ukipanga kufaulu darasani na ukafaulu kweli hayo pia ni mafanikio, kwa maana hiyo maana kubwa ya mafanikio ni KUPATA UNACHOKITAKA tu..kwa tafsiri hii asilimia kubwa ya watanzania ni failures kwa kuwa tunashindwa kupata tunavyovitaka hatimaye tunapata tusivyovitaka, haina umuhimu wa kupata kitu ambacho hakina maana wala umuhimu kwenye maisha yako, huwa tunatafuta mizigo tu ambayo inafanya safari yetu ya mafanikio kuwa ngumu.
Kwa namna yeyote ila lazima tuamini kwamba tumezaliwa kufanikiwa na lazima tufanikiwe.. wote tukiwa na spirit ya kutafuta mafanikio, kwa hakika tutayapata..haijalishi yatakuja muda gani lakini lazima tuyapate mafanikio.
Yote kwa yote MUNGU Muumbaji ndio kila kitu, YEYE ndio mwanzo na mwisho..hakika tukimtanguliza na kumshirikisha katika kila jambo tunalolifanya lazima tufanikiwe.
0 comments:
Post a Comment
Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.