Xara graphics software

07:45
1

Myles Egbert Munroe

Karibu ndugu msomaji, huu ni wakati mwingine tena ambapo tunakwenda kuangalia safari za mafanikio za watu mbalimbali, na leo tunamuangalia Dr.Myles Munroe.


Myles Egbert Munroe alizaliwa mnamo mwaka 1954, April 20 huko Nassau, Bahamas nchi iliyoko Amerika ya Kaskazini ikiwa na asilimia 80 ya watu weusi. Munroe alikulia katika familia ya kimaskini akiwa na nduguze 11 katika mji wa Bain Town. Alikulia katika mazingira ya taabu na misukosuko mingi kwani kwa wakati huo Bahamas ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza.

Munroe alibahatika kupata wokovu akiwa bado kijana mdogo saana, MUNGU alionekana kwake na mapenzi yake katika UKRISTO yaliongezeka na baadae alipata nafasi kuingia chuo kikuu cha Oral Roberts University ambapo alipata Bachelor of Fine Arts, Education and Theology mnamo mwaka 1978.

Miaka kumi na mbili iliyofuata alipata Master's degree kutoka chuo kikuu cha Tusla, kipindi hicho ndipo alipoamua kuanzisha huduma yake ya BFMI ( Bahamas Faith Ministry International ).


Myles Munroe ni moja ya wahubiri, wainjilisti na pia walimu wakubwa waliowahi kutokea kwenye hii dunia. Amekuwa msaada mkubwa sana katika maisha na imani za watu, Munroe amezunguka duniani kote akifundisha kuhusiana na Maneno ya MUNGU na maisha kiujumla, amekuwa baraka kwa watu wengi nikiwemo mimi.

Munroe pia ni mwandishi mashuhuri wa vitabu mbalimbali ambavyo aliviandika enzi za uhai wake, baadhi ya hivyo vitabu ni:
  • In Pursuit of Purpose - 1992
  • Waiting and Dating  - 2004
  • Kingdom Principles - 2006
  • Understanding your potential  - 1991
  • Releasing your potential  -  1992
  • Becoming a leader  -  1993
  • Purpose and power of Authority - 2010
  • Fatherhood principle - 2009       n.k


Ukibahatika kusoma baadhi ya makala za Munroe au kusikiliza mafundisho yake, hakika utagundua kuwa alikuwa mtu wa tofauti kabisa, alifanya kazi aliyotumwa na MUNGU aje kuifanya hapa duniani. Nimebahatika kusoma kitabu chake kimoja kinachoitwa "The Glory of Living" , kwenye kitabu hiki ameelezea mambo mengi sana ambayo kwayo humfanya mtu yeyote yule aweze kujitambua na kujua kitu cha thamani alichopewa na MUNGU wakati wa uumbaji wake.

Munroe alikuwa akitoa speeches mbali mbali katika mikutano mbalimbali ulimwenguni, mojawapo ya quotes zake ni hizi hapa:

"Because most people gravitate to illusion of security, they think there's a place or condition they can reach in life where they can stop changing. If this were possible, they would also stop growing, expanding, progressing, moving and developing."

"Don't allow negative things that occur to make you negative. Turn them into something positive and use them as a foundation for your next move. A mature person uses adversity for advancement. Allow change to move you forward in personal maturity, abilities, and skills. Use change in your life as you would discipline."

Mbali na kuwa mchungaji, motivational speaker, pia Munroe alikuwa mmja wa matajiri wakubwa huko Bahamas. Mafanikio yake yalitokana na yeye kuhusisha karama aliyopewa na MUNGU na nguvu zenye uweza wa MUNGU.

Munroe ni role model, mentor na kioo kwa watu wenye roho za mafanikio kama mimi. Hakika kazi aliyopewa na MUNGU ameikamilisha, sasa ni wakati wetu mimi na wewe msomaji kugundua vitu tulivyopewa na MUNGU kwa ajili ya kuleta mafanikio katika jamii inayotuzunguka.

Munroe alifariki Novemba 9, 2014 kwenye ajali ya ndege ya kibinafsi huko Grand Bahamas ambapo yeye na mkewe Ruth na wengine nane walipoteza maisha.
Hakika Munroe umefanya kazi yako na umeenda lakini bado unabaki kuwa mentor na kioo kwa jamii yetu, kazi ulioifanya bado inaonekana na kila mtu anaetaka mafanikio anatamani kuishi maisha kama yako yanayompendeza MUNGU na yenye mafanikio.


1 comments:

  1. Alkuwa mtu mashuhuri saana. Hakika Mungu wake ni Mkuu sana.

    ReplyDelete

Karibu Uchangie Hapa. Plant and grow creative.

Success Tips

It is always the SIMPLE that produces the MARVELOUS.....